Kikongwe mwenye umri kati ya miaka 85
hadi 90 ambaye bado hajafahamika jina lake amekutwa katika kijiji cha
Nyashimbi kata ya Muhongolo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kwa kile
kinachodaiwa kuwa huenda ni mchawi aliyeanguka usiku wakati akiwa kwenye
safari zake angani.
Kikongwe huyo baada ya kufikishwa kituo cha polisi
Kwa mujibu wa wakaazi wa Kijiji hicho
bibi huyo ameonekana leo majira ya saa 12 asubuhi akiwa katika vichaka
vilivyo kando ya barabara na alipoulizwa aliongea kidogo tu kuwa anatoka
Kijiji cha Nyihogo wilayani Kahama.
Kikongwe huyo akiwa chini huku amezingirwa na kundi la wananchi
Akiwa amelala chini kwa kile kinachodaiwa ni njaa
Alipoendelea kuhojiwa alisema alikuwa
na wenzake na vitu mbalimbali ila wamemuacha, huku akisema hawezi
kuongea zaidi kwani anahisi njaa kwakuwa alikula toka jana tena chakula
Kibichi, jibu ambalo liliwashangaza wengi ni aina gani ya chakula
ambacho huliwa kikiwa kibichi.
Bibi huyo amekutwa na nguo moja ya
Kimasai na nguo zingine chache za kawaida lakini hakukutwa na vitu
vyovyote vinavyoashiria kuwa huenda ni mchawi, hivyo kuleta hisia kuwa
huenda alikuwa ni mtembea kwa miguu tu aliyepotea njia kwani watu wote
wa eneo hilo hakuna anayemtambua.
wananchi wakimwangalia bibi kizee huyo akiwa hio bin taaban
bibi kizee huyo akiwa ameanguka chini usiku wa kuamkia leo






0 comments:
Post a Comment